Makueni Police Nab Sh.200,000 Worth Of Bhang

Polisi kaunti ya Makueni wanawasaka washukiwa wawili waliotoroka baada ya kunaswa Jana jioni wakisafirisha misokoto elfu tano ya bangi yenye thamani ya shilingi laki mbili.

Kamanda wa polisi kaunti hiyo Joseph Ole Napeiyan anasema Polisi walinasa gari hilo eneo la Kenani ndani ya mbuga ya wamanyapori ya kitaifa ya Tsavo katika barabara ya Mtito kuelekea Voi.

Anasema gari dogo aina ya Toyota Corolla iliyotumika kusafirishia bangi hiyo inazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Mtito Andei.